– Klabu ya Manchester United imeorodhesha wachezaji wawili katika nafasi ya Pogba iwapo ataelekea Real Madrid

-Mfaransa huyo amehusishwa na uhamisho wa Santiago Bernabeu

– Mchezaji wa Totttenham Christian Eriksen na wa Leicester City Youri Tielemans wametajwa

Klabu ya Manchester United imewaorodhesha wachezaji wawili mahiri sana kuchukua nafasi ya Paul Pogba huku wakiwa na hakika kuwa mfaransa huyo huenda akajiunga na Real Madrid msimu ujao.

Naibu mwenyekiti wa United, ED Woodwar, anasisitiza kuwa hatakubali saini yoyote ya kujiondoa kwa Pogba ambaye amesalia na miaka miwili kwenye kandarasi yake.

Habari Nyingine: Neymar aandikisha taarifa kwa polisi kuhusu madai ya ubakaji

Habari Nyingine: Mwanamke aliyedai kubakwa na Neymar ajitokeza hadharani

Hata hivyo, mchezaji huyo tayari yuko na nia ya kuelekea Uhispania baada ya kutangaza hapo awali kuwa yuko na azma ya kujiunga na kikosi cha Zinedine Zidane.

Kwa mujibu wa gazeti la The Evening Standard, inadaiwa kuwa tayari United wameanza mchakato wa kutafuta mrithi wa Pogba huku wakiwa na matumaini kuwa huenda akasalia Old Trafford.

Christian Eriksen bado yuko mbioni kutafuta hatima yake katika klabu cha Tottenham, baada ya klabu hiyo kuibuka kuwa mabingwa wa ligi katika nafasi ya pili msimu huu.

Habari Nyingine: Eden Hazard: Chelsea na Real Madrid waafikiana malipo

Habari Nyingine: Neymar atakosa Copa America baada ya kupata jeraha baya mguuni

Akizungumza katika mahojiano na jarida la Ekstra Bladet, Eriksen alidokeza kuwa japo anashawishiwa kusalia Uingereza kwa mkataba mpya, azma yake ni kupata mazingira mpya.

United pia wana mlenga kiungo wa kati wa Leicester City, Youri Tielemans, baada ya Mbelgiji huyo kuandikisha matokeo bora King Power.

Ole Gunnar Solskjaer, amekuwa akifuatilia matokeo ya mchezaji huyo na kufurahishwa na mechi yake ya kwanza msimu uliopita Uingereza.

Hata hivyo, timu hiyo inaazimia kuendelea kutumia huduma za Pogba huku meneja huyo raia wa Norway akimtegemea kama kifaa bora.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko