-Reno Omokri aliwaonya wanaume dhidi ya kuwaoa wanawake ambao wanapenda maisha ya kifahari

-Kulingana na Omokri, mwanamke ambaye hana kazi na amesonga nywele ya bei ya N180K atakuwa kikwazo katika ndoa

-Omokri aliwaonya wanaume dhidi ya kuoa wanawake ambao hawawezi kudhibiti mapenzi yao

Mwandishi kutoka Nigeria na ambaye pia hutumia mitandao ya jamii kutoa ushauri Reno Omokri amewashauri wanaume dhidi ya aina fulani ya wanawake.

Kwanza, alisema kwamba kumuoa mwanamke ambaye hana kazi lakini anatumia KSh 30,000 kusonga nywele atakuwa kikwazo katika ndoa.

Habari Nyingine: Bomet: Naibu Gavana kuapishwa rasmi siku 5 baada ya mazishi ya Joyce Laboso

Kulingana na mhubiri huyo, wanawake wa aina hiyo wanaenzi maisha ya kifahari tu na hawana lolote ambalo wanaweza kutumia katika kujenga familia.

Vile vile, Omokri aliongeza kwamba hamna mwanamme yeyote anayepaswa kumuoa mwanamke ambaye hajui kuthibiti mapenzi.

Habari Nyingine: Kansa ya utumbo mpana, dalili na jinsi ya kujikinga nayo

Kulingana naye, wanawake ambao hawawezi kudhibiti mapenzi yao ni kama fasheni ambayo haichukui muda kabla ya kusahaulika.

Omokri alisema itakuwa vyema mwanamme akimuoa mwanamke ambaye anampa mapenzi bila masharti kwa kuwa penzi la aina hiyo hudumu.

Habari Nyingine: DCI kukagua vyakula vinavyouzwa madukani kukabiliana na maradhi

Majuma machache yaliyopita, Omokri aliorodhesha hatua nne ambazo kulingana naye wachumba wanastahili kufuata iwapo wanataka kuoana kulingana na maandiko ya biblia.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke